NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

MAKAMPUNI YASHAURIWA KUTUMIA ‘DATA CENTRE’

Kampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zimeshauriwa kuhifadhi kumbukumbu zao katika kituo cha taifa cha kuhifadhia kumbukumbu DATA CENTRE ambacho kinatarajiwa kuanza rasmi kuhifadhi kumbukumbu mwezi Mei mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa na waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea kituo hicho cha Taifa cha kuhifadhia kumbukumbu kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo amesema itashangaza sana kwa mtanzania kwenda kuhifadhi kumbukumbu nje ya nchi wakati tayari taifa limeshaanzisha kituo cha kisasa kwa madhumini hayo

Profesa Mbarawa amesema katika biashara ya vituo vya kuhifadhi kumbukumbu, kituo hicho ni kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati.

Aidha Profesa Mbarawa amaesema serikali ina mpango wa kujenga vituo vingine viwili vya kuhifadhia kumbumbu katika mkoa wa Dodoma na Zanzibar huku akiwahakikishia wananchi na wadau mbalimbali kuwa kumbumbuka hizo zitahifadhiwa katika hali ya usalama bila usumbufu wowote.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment