Hali
ya sintofahamu imeibuka katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount
Meru baada ya mtoto mchanga wa siku tano kuibiwa wodini katika mazingira
ya kutatanisha.
Tukio
hilo limezusha hofu kwa baadhi ya wazazi waliojifungua katika wodi ya
wazazi hospitalini hapo wakihofia usalama wa watoto wao na kuomba
Serikali kuingilia kati.
Akisimulia
tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Sinyari Lucas ambaye ni mkazi wa
Simanjiro mkoani Manyara, alisema lilitokea usiku wa kuamkia jana.
Akizungumza
huku akiwa ameghubikwa na huzuni, Lucas alisema wakati akiwa kitandani
muda wote kabla ya kulala alikuwa na mtoto wake.
Mumewe, Lucas Ngaraa alionyesha kushangazwa na tukio hilo kwa sababu hospitali hiyo ina ulinzi wa kutosha.
Baadhi
ya wazazi waliokuwapo kwenye wodi hiyo, walisema muda wote mzazi huyo
alikuwa amelala kitandani na mtoto wake, lakini usiku walishangaa
kumsikia anapiga kelele.
Mganga
Mkuu Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Jackline Urio alikiri kuwapo kwa
tukio hilo na kwamba, uongozi umelipokea kwa mshtuko mkubwa na
unalifanyia kazi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema wamepokea taarifa
hizo na tayari ameagiza maofisa kwenda kufuatilia tukio hilo kwa kina.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment