Machi 13 mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
-
Mh. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
-
Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
-
Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
-
Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
-
Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
-
Mh. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
-
Dkt. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
-
Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
-
Mh. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
-
Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
-
Mh. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
-
Mh. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
-
Mh. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
0 comments:
Post a Comment