NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

WATOTO WALEMAVU WADAIWA KUKOSA UPENDO KWA WAZAZI WAO


 
WATOTO  wenye ulemavu mbalimbali  409  wanaolelewa katika kituo jumuishi kilichopo Buhangija Manispaa ya Shinyanga wamedaiwa kukosa upendo dhidi ya wazazi  na walezi  kwenye familia zao baada ya kuwatelekeza kwa muda mrefu.

Kwani wazazi wamekuwa hawatoi ushirikiano dhidi yao hata katika kipindi hiki cha sikukuu ya pasaka wameshindwa kujitokeza nakuwafarij huku wakikubwa na changamoto ya uhaba wa mavazi na  mlo kamili.
 
Hayo yalisemwa jana na  mwalimu  Sasu Nyanga  msaidizi msimamizi wa kituo hicho baada ya familia ya muuguzi mstaafu  Anna Mwalongo na mumewe Josephat Mwalongo kutoa msaada wa nguo,kilo 100  za mchele na  mbuzi mmoja  katika kituo hicho.
 
Nyanga alisema kuwa kituo hicho kwa sasa kina jumla ya watoto  409 aliwataka wazazi na walezi wajenge upendo kwa watoto hao kwani  wameonekana  kukosa  upendo  kwasababu ya kushindwa kutoa ushirikiano tangu wanapowaleta  na kwenda moja kwa moja bila kurudi nakuwajulia hali zao.
 
“Kituo hiki kinawatoto  wakuanzia miaka miwili hadi  12  wakiwa  70 wamekosa upendo wa dhati kwa  wazazi wao kwani tangu wamewaleta kituoni hapa wameshindwa kurudi  kuwajulia hali  nakuwafariji hasa Kipindi hiki cha  sikukuu ya pasaka pia wana changamoto ya kukosa  mavazi,chakula na malazi”alisema mwalimu Nyanga.
 
Anna Mwalongo ambaye ni muuguzi mstaafu  na msemaji kwa niaba ya familia yake alisema kuwa wameguswa kutoa msaada wa vitu hivyo kutokana na watoto hao wenye haki ya kupata stahiki zote kama binadamu wengine  wapate hasa kipindi hiki cha sikukuu ya pasaka.
 
Hata hivyo waliendelea kutoa msaada wa nguo  katika kambi ya kulelea wazee wenye maradhi ya ukoma wapatao 23  ambao wanachangamoto ya mavazi  pia aliwaomba wadau wengine wasiishie  msaada wa vyakula bali waangalie na changamoto zingine zinazowakabili wazee hao ni nyingi.
 
Baadhi ya wazee hao Hellen Masanja na Shija  Nipuge walishukuru msaada huo huku wakieleza changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme,nyumba kuwa na nyufa na kuvuja kipindi cha mvua ikiwemo kukosa matibabu
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment