Siku Mh Anna Kilango Alipokuwa anaapishwa |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
mchana huu ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna
Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake
hauna wafanyakazi hewa wakati kumbe wapo wengi tu.
Rais
Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna
wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa
kuamkia leo kimebaini kuweko na wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.
Rais
Magufuli, ambaye alikuwa anaongea baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU
toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu Valentino Mlowola, amesema kasikitishwa
sana na kauli ya Mama Malecela ambaye bila shaka alikuwa amepata
ushauri mbaya toka kwa watendaji wake.
Amesema
idadi hiyo ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka
zaidi kwani wilaya mbili zilikuwa bado zinaendela kuhakikiwa.
Rais
Magufuli amesema pia kwamba hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi
ya 5, 507 wamebainika nchi nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri.
Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita.
Katika
siku hiyo Rais aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe
katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote
katika halmashauri zote nchini, na kuwataka wakuu wa Mikoa hao wasimamie
zoezi hilo kwa ukamilifu.Vile
vile Rais Magufuli alionya kuwa halmashauri yoyote baada ya muda huo
itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake atakuwa amejifuta kazi
mwenyewe.
Vilevile
Rais amewaagiza mawaziri wote kuwaeleza watendaji wao wawaondoe
wafanyakazi hewa wote ndani ya kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha
kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria
ni msumeno.Chanzo Issa michuzi Blog
SHARE
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook
, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment