NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Hatimaye Leicester City yafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA

Leicester-City-v-West-Ham
Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza, Leicester City imejihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA kwa mara ya kwanza baada ya kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila dhidi ya Sunderland.
Magoli ya Leicester katika mchezo huo yote mawili yalifungwa na Jamie Vardy katika daika ya 66 na 90 na hivyo kuiwezesha Leicester kufikisha alama 72 ambapo zimewawezesha kupata nafasi ya kushiriki mashindano makubwa kwa vilabu Ulaya.
Mara ya mwisho kwa Leicester kushiriki mashindano yanayoandaliwa na UEFA ni mwaka 2000-2001 ambapo ilishiriki mashindano ya UEFA Cup.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment