LICHA
ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto
mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine ametengeneza habari,
amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar
Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
PICHA ZADHIHIRISHA
Hiyo imedhihirika hivi karibuni
baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika
mapozi ya kimahaba huku wamevaa mavazi ya kulalia (angalia picha Uk. 1).
Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz
akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono
kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilicho karibu na
Dimpoz, kimepenyeza habari kuwa, licha ya Wema kupitia uhusiano tofauti,
Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa siri jambo ambalo watu wengi
hawalitambui.
“Mbona kitambo tu, Dimpoz
amejiweka kwake kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo hayo kwa siri. Si
mnajua Dimpoz si mtu wa kutangazatangaza mambo yake na ndiyo maana hadi
Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya
hadi kumuimba kwenye wimbo wake,” kilisema chanzo.
MAZINGIRA YA TUKIO
Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa,
picha hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani kwa Dimpoz, Kinondoni
jijini Dar hivyo zilibaki katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho
kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi wetu.
“Bwana nakupa lakini msinitaje
huko, nyie kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo hiyo; Dimpoz na
Wema ni kapo ya kimyakimya maana wenyewe hawataki kuanika mambo yao,”
kilisema chanzo hicho.
AKUMBUSHIA BIFU LA DIAMOND
Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi
kuwa, kutokana na Diamond kufahamu kuwa, wawili hao wanaendeleza
uhusiano, ndiyo maana tangu picha zao za awali zilipovuja mwaka jana
wakiwa nchini Afrika Kusini, Diamond na Dimpoz haziivi na hata
uswahiba haupo tena kama zamani zile.
“Diamond hataki hata kumsikia
Dimpoz katika maisha yake, anamuona ni mtu ambaye hakufanya uungwana
kuwa na mtu ambaye yeye tayari ameshatembea naye,” kilisema chanzo
hicho.
WEMA ASAKWA
Baada ya kupata ubuyu huo,
mwanahabari wetu ‘alimvutia waya’ Wema ili kumsikia anazungumziaje picha
hizo na uhusiano huo unaodaiwa ni wa siri, simu yake iliita bila
kupokelewa lakini baadaye rafiki yake mmoja alisema huenda hakupokea kwa
kuwa siku hiyo alikuwa safarini kuelekea Dodoma.
“Jana (Jumatano) aliniaga ana
safari ya Dodoma so (hivyo) nafikiri yupo njiani na wenzake na pengine
kelele za wasanii ndani ya gari si unajua tena na kaenda na wasanii
wenzake wengi tu,” alisema rafiki huyo ambaye hakupenda jina lake
lichorwe gazetini.
DIMPOZ HUYU HAPA
Baada ya kumkosa Wema, mwanahabari
wetu alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha hizo zilikwapuliwa
kutoka kwenye simu yake lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.
“Hizo picha nazijua, nakumbuka
tulipiga hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si nyumbani kama huyo mtu
alivyowaambia lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua, Wema ni mshikaji
wangu wa karibu na hakuna kitu kingine zaidi ya ushikaji. Kuna mtu
itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini nitadili naye lazima
nitamjua tu,” alisema Dimpoz.
KUMBUKUMBU
Wema na Dimpoz walidaiwa kuanzisha
uhusiano wa kimapenzi, Februari, mwaka jana walipokuwa wakirekodi video
ya Ommy, Wanjera nchini Afrika Kusini.
Picha zao ‘tata’ wakiwa chumbani zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa katika vyombo vya habari.
Baada ya hapo, Wema aliripotiwa
kutembea na wanaume tofauti akiwemo Idris Sultan, mshindi wa Shindano la
Big Brother Africa-Hot Shot (2014).
Chanzo:Global Publishers
0 comments:
Post a Comment