Unaambiwa raha ya penzi ujue kuenzi, Je
mpenzi wako unamfurahisha kwa mambo yapi? basi leo nikuibie siri Jinsi
ya Kumfurahisha Mwanaume wako katika mahusiano yenu.
1.Mlishe au jenga mazoea ya kula pamoja nae,
Hivi wewe hapo ukilishwa huwa unajisikiaje? Bila shaka jibu ni raha
tupu asikwambie mtu mwanaume ni kama mtoto jitahidi kuenda nae sawia kwa
mahaba haya akikuacha basi huyo ujue kivuruge.
Kuna wengine hudai kuwa wanaostahili
kulisha ni wale wanaotembea na waliowazidi umri la hasha! Utafeli dada
wewe utaishia kuambiwa niko bize na kazi tutaonana wikiendi.
2.Kuwa karibu nae,
Unapoanzisha uhusiano ujue kabisa kile ni kitendo kisichokuwa cha hiari
jitahidi mara moja moja unamridhisha mwenzi wako sio kila siku uko bize
na shughuli za hapa na pale wenzio wakichangamkia fursa ujue itakula
kwako na usiposhtuka mapema utajikuta unasubiri Meli Airport.
3.Ishi nae kwa Amani,
Kuna watu wanajikuta wanataka kubembelezwa tu pasi na sababu atatafuta
sababu ilimradi tu atake kujua kwamba akimuudhi mpenzi atachukua uamuzi
gani, angalia kuna wengine hawajui kubembeleza kwa kingereza tunawaita
“UNROMANTIC MEN” yaani huyu ukimzingua tu inakula kwako.
4.Usichunguze Simu yake,
Mahusiano ya kipindi hiki cha utandawazi yamegeuzwa thamani yake kuwa
ni sawa na utamu wa bazoka unatafuna ikiisha utamu unatema lakini chanzo
cha yote ni simu za mkononi kwani zimechochea sana usaliti hasa huu
mtandao ulioteka vijana wa sasa “Whatsapp” mtu akitumiwa picha tu hata
mtu hujawahi kumuona ushaingiwa tamaa.
Ili kuepukana na presha zote hizo achana
na kukagua simu ya mwenzi wako yaani kwa lugha nyepesi acha shobo na
simu ya mwenzio maana isije kuwa chanzo cha kuhatarisha uhusiano wako na
wanaume wengi hawapendi kwa kuzingatia hilo atakupenda mno.
5.Usimsumbue na Mizunguko yake,
Kuna wanawake wengine huwa wanaboa sio siri kwa hili badilikeni mtu
atataka ajue unaenda wapi na unafanya nini na uko na nani tena wengine
hufika mbali “ooohooo uko na nani mbona huongei kwa kujiachia hebu ni
kiss nijue kama hauko na mwanamke” tambua yule ni mtu mzima anamajukumu
yake sio kila kitu akwambie vingine kubali vikupite asikudanganye mtu
mwanaume hapendi kufatiliwa kupita kiasi.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
JINSI YA KUMFURAHISHA MWANAUME WAKO
Reviewed by Newspointtz
on
13:08:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment