
Kiungo
wa Tottenham Hotspur, Mousa Dembele amepewa adhabu ya kutokucheza
michezo sita na Chama cha Soka Uingereza kwa kumkwaruza katika jicho
mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa wakati timu hizo zilipombana
Jumatatu iliyopita.
Kocha
wa Tottenham, Mauricio Pochettino amethibitisha Dembele kupewa adhabu
hiyo ambayo itamfanya kukosa michezo iliyosalia ya msimu huu na mingine
ya msimu ujao utakaoanza mwezi Agosti.
Tottenham
imebakiza michezo miwili hivyo Dembele ataukosa mchezo wa Southampton
na Newcastle United na michezo mingine minne itakuwa ya msimu wa
2016/2017.
0 comments:
Post a Comment