
Mshambuliaji
chipukizi wa Manchester United, Marcus Rashford amezidi kupata umaarufu
kutoka kwa wanamichezo wakubwa duniani pamoja na wadau wa michezo na
kwa sasa amepata sifa kutoka kwa staa mwingine, Ronaldo.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil amesema kuwa
uwezo wa Rashford ni mzuri kulinganisha na umri wake.
Ronaldo
amesema uwezo alionao Rashford niwa kiwango cha juu na namuona kama
mchezaji ambaye anaweza kuja kuchukua nafasi yake kwa kuwa na baadhi ya
vitu ambavyo alikuwa akivifanya wakati wa enzi zake.
“Ni
mchezaji mdogo lakini mwenye uwezo, ninaona baadhi ya vitu
nilivyokuwanavyo vikiwa ndani yake, ni jasiri na anakuwa na kasi
anapokuwa na mpira,
“Napenda
washambuliaji ambao wana hasira na magori na hilo analo, naamini
atakuwa na wakati mzuri katika maisha yake ya kucheza soka,” Ronaldo
aliliambia gazeti la The Sun.
0 comments:
Post a Comment