Snura amewaonesha kile alichosema ni cheti.
Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake
wa Chura ulipigwa marufuku na serikali ya Tanzania jana ameomba radhi na
kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali.
Wimbo huo ulipigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilisema "maudhui ya utengenezwaji wa video ya wimbo huo “haiendani na maadili ya Mtanzania.”
Mamlaka hiyo ilisema kazi hiyo inadhalilisha tasnia ya muziki.
Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi pale atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
Share !
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook
, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment