NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Belle 9: Watu wameponda mtindo wangu wa nywele lakini nimejifunza kitu


IMG-20160603-WA0005
 Belle 9 amesema kuwa pamoja na mashabiki kuponda mtindo wake mpya wa nywele (bleach) amejifunza kitu muhimu kupitia maoni yao.

Staa huyo amesema kuwa amejifunza kuwa anaangaliwa sana na kila anachokifanya kina impact kubwa kwa mashabiki wake.

Amedai kuwa licha ya kupata mrejesho hasi, hajisikii vibaya kwakuwa yeye ni mtu anayependa fashion na kuwa tofauti mara zote. Muimbaji huyo ameongeza kuwa kama msanii amekuwa akijitahidi kuwa tofauti kila mara huku akiwatolea mfano wasanii wa nje akiwemo Chris Brown kuwa nao wamekuwa wakifanya hivyo.

Belle ambaye anatarajia kuachia remix ya wimbo wake Bulger Movie Selfie (BMS), amesema watu wasishangae baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan akaja tena na mtindo mpya wa nywele.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment