NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Dr Dre na 50 Cent washtakiwa kwa mdundo wa P.I.M.P


image
 50 Cent na Dr. Dre wanashtakiwa kwa kutumia beat ya producer mwingine kutengeneza wimbo, P.I.M.P.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka TMZ, Brandon Parrott anadai kuwa wimbo wake ‘BAMBA’ ulitumika kwenye wimbo huo wa tatu wa 50 Cent kutoka kwenye album yake ya kwanza,  Get Rich Or Die Tryin ya mwaka 2003 bila ruhusa.

Kwa mujibu wa Parrott, aliwasilisha nyimbo 10 kwenye label ya Dr. Dre, Aftermath Entertainment mwaka 2001 — ukiwemo ‘BAMBA’ — kwa lengo la beat zake kuchaguliwa kwaajili ya wasanii wa label hiyo.

Parrott pia anadai kuwa producer mmoja wa Dr. Dre alimtafuta wakati album hiyo ikimaliziwa na kusema kuwa walitumia beat hiyo bila kupanga. Matokeo yake, alisaini makubaliano ya kutajwa kushiriki kutayarisha beat ya P.I.M.P.

Na sasa Parrott anadai kuwa taarifa hiyo si ya kweli na anamshtaki 50 Cent na Dr. Dre apewe fungu lake kutoka kwenye faida iliyopatikana kupitia ngoma hiyo.

Hata hivyo producer huyo anaweza asipate kitu kutoka kwa 50 Cent anayeandamwa na madeni kibao huku akiwa amejitangaza kufilisika. Labda atapata chochote kwa  Dr. Dre ambaye hadi sasa ni rapper wa tatu kwa utajiri.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment