
Professor Jay akiwa na msanii wa WCB, Raymond
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini na mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ baada ya kutembelea makao makuu ya label ya WCB hivi karibuni, amegundua wasanii wa label hiyo wana nidhani ya hali ya juu.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amesema amewakuta wasanii wa WCB wana nidhamu ambayo ni tofauti na wasanii wengine.
“Nimeenda pale nimekuta kuna nidhamu ya hali ya juu, yaani wale wasanii hawaruhusiwi kutoka nje ya geti bila ruhusa maalum, ukimuona nje ametumwa na ofisi au ametoka kwa ruhusa maalum,” alisema Professor. “Hii inatengeneza brand ya mtu, msanii huwezi leo ukaonekana Buguruni, mara leo yupo Tandale. Wasanii wengi hafanyi vitu kama hivi, mtu anakuwa na talent lakini anashindwa kuilinda talent yake, ili kulinda image msanii hatakiwi kuonekana mara kwa mara amezagaa zagaa kama hawana shughuli ya kufanya,”
Aliongeza,”Wasanii wanatakiwa wajifunze kwamba, kama huna shughuli ya kufanya hauna sababu ya kuzagaa barabarani, pata muda tafakari, jifunze ili uweze kufanya vizuri zaidi. hiyo nimeikuta WCB, wasanii wapo busy kuandika na kufikiri kuhusu kazi zao, pongezi sana kwa uongozi, Saidi Fella na Babu Tale kwa kuwajenga vijana, kazi yoyote ni nidhamu. Wasanii wanadhani wanafanya wote lakini wanashindwa kugundua muziki ni kazi, na inahitaji nidhamu ya hali ya juu na wajifunze kutoka kwa wengine,”
0 comments:
Post a Comment