
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius Jumatano hii
amelazimika kutoa miguu yake ya bandia ili kumuonesha jaji jinsi alivyo
dhaifu na kwamba asingeweza kumuua mpenzi wake makusudi.
Kwenye kesi hiyo iliyokuwa ikioneshwa live kwenye TV, mwanariadha huyo alijaribu kutembea kwa tabu bila miguu hiyo.

T-shirt yake ilikuwa imeloa kwa jasho na macho kuwa mekundu kutokana na kulia.

Pistorius anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi pale jaji atakapotangaza tena tarehe ya hukumu.
0 comments:
Post a Comment