NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Rama D na Lady Jay Dee vipiiiii?

 

                                                            Rama D na Lady Jay Dee

Mwanamuziki wa R&B nchini Tanzania Rama D, amekanusha vikali habari zilizotapakaa mtandaoni kwamba kwa sasa anatoka kimapenzi na mwanadada Lady Jay Dee, amesema wanaheshimiana sana na haiwezi kutokea kitu kama hicho daima .
                                                       
Hata hvyo Rama D ameendelea kusema kwamba yeye anamfaham mpaka mpenzi wa mwanadada Lady Jay Dee na kusema hata siku ya show ya 'Naamka Tena Concert' alipanda jukwaani kuonesha jinsi anavyomkubali mwana dada huyo.

Rama D anasema anawashangaa sana watu wanaoenda kufanya video zao nje na kusema kwamba haoni sababu ya kufanya video hizo nje kwani hapa nyumbani kuna mazingira ya kutosha kufanya video nzuri zitakazoitangaza nchi.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment