
Msanii Iqbar Mohamed Bagati.
mkali wa Bongo Alikiba na Naijaa Davido na Wizkid ndio wasanii wakubwa mno katika Jiji la Lubumbashi kwa sasa.
Mohamed ambaye yupo nchini kwa lengo la kutengeneza ‘connection’ na wasanii wa kibongo, amedai kuwa AliKiba
‘Kiba 4 Real’ anayetesa na ngoma yake ya Aje kwa sasa anaweza kujaza uwanja wa mpira kwa siku tatu mfululizo
kulingana na jinsi anavyokubalika huko Lubumbashi.
Amesema mkali huyo wa Bongo ni kipenzi cha wakongo wengi sana hususan akina dada.
“Alikiba anawashinda Davido na Wizkid, nap engine tunaweza kumlinganisha na akina P-Square huko
Lubumbashi ambapo kwa upande wa Davido aliwahi kutumbuiza kama mara nne hivi huko Lubumbashi
huku P-Square wakitumbuiza kama mara mbili tu,” amesema.
Akielezea umaarufu wa Kiba, Mohamed amedai kuwa kama msanii huyo ataamua kwenda leo Lubumbashi
basi atashangaa sana kwa mapokezi makubwa atakayoyapata katika Jiji hilo ambalo ndipo maskani mwa
klabu ya soka ya TP Mazembe na wakazi wengi wa eneo hilo wakiongea Kiswahili.

0 comments:
Post a Comment