RAIS John Magufuli amesema watu
wanaolalamika kwamba fedha hazionekani mitaani ni watu waliozoea ‘kupiga
dili’ (kujipatia fedha isivyo halali).
Ameeleza kuwa wapo wananchi walioficha
fedha ili wasibainike kuwa na kiwango kikubwa na kuwataka wazitoe,
vinginevyo anaweza kuchapisha noti mpya na hizo zilizofichwa zikaoza.
Akifungua Mkutano wa 14 wa Siku ya
Wahandisi nchini uliofanyika Dar es Salaam jana, Dk Magufuli alioneshwa
kukerwa na tabia ya watu waliozoea, kuifanya nchi kama shamba la bibi
kwa kutapanya mali za umma huku baadhi ya watendaji wakikiuka maadili ya
uongozi kwa maslahi binafsi.
“Tanzania imechoka kuibiwa na kuchezewa
kwa sababu kila mahali ni dili, ukigeuka huko wanapiga dili, huku ni
dili, serikali kupitia mashirika ya umma mbalimbali ilikuwa haipati hela
kwa sababu ya dili, ni dili tu kila mahali, sasa kwa mwendo huu wa
kwangu hizo dili basi,” alisisitiza Rais Magufuli.
Akizungumzia wananchi walioficha fedha,
Rais Magufuli aliwataka wazitoe fedha hizo na ziende kwenye mzunguko wa
fedha na kwenye miradi ya maendeleo, na kusisitiza kuwa anaweza kuamua
kubadilisha noti na hizo zilizofichwa zikawaozea kwenye magodoro.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
JPM-WATU WALIZOEA ‘MADILI ‘ SANA
Reviewed by Newspointtz
on
09:42:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment