SERIKALI imesema itafanya mapinduzi
makubwa katika sekta ya sheria, yatakayowezesha kufikiwa kwa mchakato wa
Katiba Mpya, kukomesha rushwa, kuipa meno Sheria ya Ndoa na Mirathi na
kuipa majukumu Mahakama ya Rushwa na Mafisadi.
Maeneo mengine yatakayofanyiwa kazi ili
kuboreshwa ni Sheria ya Mitandao, Sheria ya Kupata Taarifa, lakini pia
kupelekwa bungeni kwa Muswada wa Sheria ili kuwasaidia wananchi wasio na
uwezo wa kupata huduma za kisheria.Hayo
yalisemwa juzi usiku na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison
Mwakyembe wakati akizungumza katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’
kinachorushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha TBC1, kwa lengo la
kuainisha shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali katika
kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Katiba Mpya Inayopendekezwa
Akizungumzia Katiba Mpya
Inayopendekezwa, Mwakyembea alisema mchakato wa kupata Katiba mpya ya
Tanzania, ambao uliachwa kiporo na Serikali ya Awamu ya Nne, upo pale
pale ingawa utekelezaji wake utakwenda polepole.
Alisema uthibitisho kuwa mchakato huo,
utaendelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kauli iliyotolewa na Rais
John Magufuli mara kadhaa kwamba serikali yake itaendelea na mchakato
huo ili kupata Katiba mpya.
“Na mimi (Mwakyembe) niseme vivyo
hivyo, nina uhakika kuwa litafanyika hivyo, alichokifanya Rais ni kuzipa
nguvu mamlaka husika ili kuendelea na mchakato huo bila kuingiliwa,”
alisema Dk Mwakyembe.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MWAKYEMBE- KATIBA MPYA INAKUJA
Reviewed by Newspointtz
on
09:44:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment