Chadema imetaja sababu tatu za
kuahirisha kwa mwezi mmoja mpango wake wa kuandamana na kuendesha
mikutano ya hadhara kote nchini kuanzia leo, kuwa ni kutoa nafasi kwa
viongozi wakuu wa dini kuzungumza na Rais John Magufuli kutafuta suluhu
ya kudumu ya madai yao.
Hata hivyo, Chadema imesema uamuzi wao
wa kuahirisha maandamano na mikutano hautokani na vitendo vya kukamatwa
kwa viongozi wa chama hicho, Polisi kufanya mazoezi ya wazi hadharani,
Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutangaza Septemba Mosi kuwa siku ya usafi
wakati ilishafanya Julai 25 na kauli za vitisho za viongozi wa Serikali.
Uamuzi wa kuendesha mikutano na
maandamano kote nchini ulifikiwa na Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana
kwa siku mbili jijini Dar es Salaam na kutangazwa Julai 27.
Jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya viongozi kadhaa wa
dini, mke wa Baba wa Taifa na taasisi nyingine kuongea na viongozi,
chama hicho kimeamua kuahirisha uzinduzi wa harakati hizo kwa siku 30
ili wakuu hao waweze kuzungumza na Rais John Magufuli na Serikali yake.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
UKUTA MIKONONI MWA JPM
Reviewed by Newspointtz
on
08:39:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment