NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Baraza La Wazee Chadema Lamuombea Dua Rais Magufuli

Rais Dk John Magufuli.
Rais Dk John Magufuli.
Katika Hali ya kuonesha uzalendo licha ya tofauti za kisiasa  Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limejitokeza na kumuombea dua Rais John Magufuli awe na afya njema.
Dua hiyo ilitolewa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma katika mkutano na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza namna ambavyo hawaridhishwi na mwenendo wa utendaji kazi wa Rais Magufuli na yaliyojiri Zanzibar.
Hashim alisema pamoja na kwamba baraza hilo haliridhishwi na mwenendo wa Rais Magufuli, limeamua kumuombea dua kwa sababu rais mwenyewe aliomba kuombewa.
“Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema, ampe maisha marefu na amjalie aongoze katika misingi anayopenda yeye, amina,” alisema Hashimu wakati akiongoza dua na wazee wengine kuitikia amina.
Baada ya kukamilisha dua  Hata hivyo wazee hao  waliituhumu serikali ya Magufuli  kuwa  inakandamiza upinzani na pia haendeshwi katika misingi ya kidemokrasia.
Alisema Rais Magufuli amekuwa na kauli tata ambazo amekuwa akizungumza hadharani lakini viongozi na wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kukemea na wao hawawezi kukaa kimya.

Hashim alisema baraza hilo linamshauri Rais aunde kamati ya wazee wa kumshauri ambao atakutana nao walau mara nne kwa mwaka kutoka mikoa yote na ikizingatia jinsia.
Alisema baraza hilo linamshauri pia rais ashughulikie kupatikana kwa Katiba ya nchi, na mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa, “bila kupatikana katiba mpya ufisadi ambao anaupiga vita hautaisha,” alisema Hashim.
Aidha baraza hilo lilimtaka rais kuingilia kati mgogoro wa wabunge wa upinzani waliosusa vikao vya Bunge ili warudi bungeni.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment