Umewahi kufikiria ama kujiuliza faida zinazopatikana kwa kumkumbatia mkeo ama mpenzi wako mkiwa mmelala? newspointtzcom inakufunulia Katiba Uwanja wa Mahaba ili upate kufahamu yale yanayokupa faraja ya penzi kutokana na kumbatio karibu twende sawa.
HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA
Unapomkumbatia mkeo ama mpenzi wako
mkiwa mmelala husaidia kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho
‘oxytocin’. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na
maradhi ya moyo na hupunguza shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia
hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu ya kichwa na maradhi
mengine.
USINGIZI MARIDHAWA
Wanandoa wanapokumbatiana husaidia
kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza ‘cortisol’
na hivyo hupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi ‘cortisol’
inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana.
Unapomkumbatia mwandani wako
huleta raha, hasa mambo yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini
kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga
mbele… moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano
huo ili kujenga uaminifu na hisia za ushirika.
MAWASILIANO BILA MANENO
Kukumbatiana hutoa fursa kwa wapenzi ya
kuwasiliana bila kuongea. Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa
kuzidi kuwa karibu.
NI DAWA YA FADHAA
Kimbilia kitandani ili kupata kumbatio
la asali wako wa moyo; kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo.
Achana na kitabu, televisheni, simu, tablet na mambo mengine kama
hayo. Kumbatio litakusaidia kumakinika na kupata utuvu.
HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA
Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la
kuingia kweye tendo la ndoa, mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa
yenu. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana
wanaridhika sana na ndoa zao kuliko wale wasiokumbatiana.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Umuhimu wa kumbatio(HUG) kwa mpenzi wako
Reviewed by Newspointtz
on
09:08:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment