Wanawake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA), wamesema kuwa licha ya kurejea katika vikao vya bunge baada ya
kususia ila msimamo wao wa kujiondoa katika umoja wabunge wanawake upo
pale pale.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Halima Mdee, amesema kuwa tayari wameshaandika barua kwa Naibu Spika
kuhusiana na suala hilo na wanasubiri maamuzi yake.
Mdee amesema kuwa wameamua kufanya
hivyo baada ya kuona umoja huo ambao ulitakiwa kukemea matendo ya
udhalilisha kwa wabunge wanawake haujalipa uzito wa suala hilo ambalo
limeelekezwa kwa wabunge wanawake wa vyama vya upinzani.
Pia amesema kuwa hatima yao ya kurudi
katika umoja huo wa wabunge wanawake itategemea na Naibu Spika ambae pia
ni kiongozi katika umoja atajibu nini na baada ya hapo watakaa kujadili
ni jinsi gani wataweza kushirika katika umoja huo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Wabunge ukawa warjea Bungeni kwa masharti
Reviewed by Newspointtz
on
09:11:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment