NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Bodi ya Mikopo imevurunda sana - Prof. Ndalichako

 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojiana Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ametoa wiki mbili kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini kuwachukulia hatua watumishi wa bodi hiyo aliowasimamishwa kazi Februari 16 mwaka huu.

Watumishi hao walisimamishwa kazi kutokana na udhaifu uliobainika katika mfumo wa usimamizi wa fedha, utoaji na urejeshaji wa mikopo ya wanafunzi.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Prof Ndalichako, amesema, aliiagiza ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG ambayo imeonesha mapungufu mengi na kuonesha tuhuma 17 zinazowakabili watumishi hao na kuamua kutoa maagizo kwa bodi hiyo kuunganisha mfumo mzima wa kuainisha wanafunzi waliokopeshwa na wanafunzi wanaodaiwa ndani ya wiki mbili.

Prof. Ndalichako ameongeza kuwa wanafunzi 2,616 wamelipiwa katika vyuo viwili tofauti zaidi ya Shilingi Bilioni 14.4  na kusababisha hasara kwa serikali.

Amesema wanafunzi 168 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wanafunzi 919 wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM. hawatambuliwi na vyuo hivyo licha ya kuwa wamepewa mikopo.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment