
Michuano ya Euro 2016 imeendelea tena mchana wa leo kwa mchezo
uliowakutanisha wana ndugu wawili kutoka katika himaya ya Malkia
Elizaberth: England vs Wales.
Kabla
ya mchezo wa leo, Wales ambao walikuwa wamepoteza mechi zao 4
zilizopita dhidi ya England walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda,
lakini bado wameendelea kuwa wateja wa ndugu zao, baada ya kukubali
kipigo cha 2-1 jioni ya leo.
Gareth Bale alianza kuifungia Wales kwa goli zuri la mkwaju wa faulo
ambao ulitinga wavuni baada ya kumshinda Joe Hart dakika ya 42 ya
mchezo.

Kipindi
cha pili kocha Roy Hodgson akasawazisha makosa yake kwa kufanya sub
nzuri ya kuwaingiza Daniel Sturridge na Jamie Vardy, ambao
hawakumuangusha kocha wa baada ya kushindilia misumari miwili na kuipa
England ushindi wa kwanza na muhimu katika kundi B ambal sasa wanaongoza
wakiwa na pointi 4.

Kwa
upande mwingine kijana Marcus Rashford ameweka rekodi ya kuwa mchezaji
mdogo zaidi kuwahi kuicheza katika michuano ya Euro, leo aliingia dakika
takribani 10 za mwisho badala ya Adam Lallana.

Uingereza
sasa wamejiweka mahala pazuri wakisubiri mchezo wao wa mwisho dhidi ya
Slovakia ambao jana nao walishinda kwa kuwafunga Russia ambao sasa
wanashika mkia kwenye kundi lao.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia
Facebook
,
Twitter na
Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment