NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Tiwa Savage rasmi ndani ya label ya Jay Z, Roc Nation

13395042_258480814510763_1354213566_n
  Muimbaji wa Nigeria, Tiwa Savage amekuwa msanii mpya wa label ya Jay Z, Roc Nation.
Jay Z, Tiwa Savage na Don Jazzy
Hatua hiyo imethibitisha tetesi hizo zilizoanza kusemwa kuanzia wiki mbili zilizopita kwa picha aliyoiweka Tiwa kwenye Instagram akiwa na bosi wake mpya Jay Z na yule wa sasa, Don Jazzy.
Tiwa Savage bado ni msanii wa Mavin Records ya Don Jazzy huku Roc Nation ikimsaini kwaajili ya kumweka kwenye ramani ya kimataifa zaidi hususan Marekani.
13402588_1756296114616088_93892427_n
Tiwa Savage na Don Jazzy walikutana na Jay Z kwenye makao makuu ya Roc Nation jijini New York Marekani.
Balozi huyo wa Forte Oil, MTN na Pepsi atakuwa msanii wa kwanza kutoka Nigeria kusainishwa kwenye label hiyo na kujiunga na Rihanna, Big Sean, DJ Khaled na wengine
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment