NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Zitto Kabwe afikishwa kituo cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa


Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewasili katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam ikiwa ni kuitikia wito wa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Zitto Kabwe amefika kituoni hapo leo asubuhi baada ya kutakiwa kufika kwa ajili ya kuhojiwa kufuatia kauli kadhaa alizozitoa siku ya Jumapili Juni 5, alipokuwa akihutubia wananchi katika viwanja wa Zakhem Mbagala.

Inaelezwa kuwa, Zitto Kabwe alitoa kauli ambazo zinaelezwa ni za kichochezi. Katika mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu ya “Linda Demokrasia nchini”, Zitto Kabwe alikaririwa akisema kuwa nchi inaelekea kuingia kwenye udiktea.

Zitto Kabwe ni miongoni mwa wabunge 7 waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda tofauti kutakana na kile kilicholezwa kuwa walifanya vurugu Januari 27, 2016 wakijadili suala la kurusha matangazo ya bunge ;Live’
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment