NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Video: RONALDO ALIMNYIMA JEZI NAHODHA WA ICELAND

Nahodha wa Iceland Aron Gunnarsson anajivunia kuliongoza taifa lake kupata sare ya kufungana bao 1-1 na Ureno, na kupata pointi moja kwenye mashindano ya Ulaya waliyoshiriki kwa mara ya kwanza. Lakini baada ya mchezo huo kumalizika, badala ya kwenda kwa mashabiki kuwashukuru kwa sapoti yao na mafanikio wanayopata, Gunnarsson alifikiria kitu ambacho kinaweza kikampa kumbukumbu na ndipo alimfuata Cristiano Ronaldo na kuomba wabadilishane jezi. Ilimchukua Gunnarsson kama dakika moja au mbili hivi kumfanya Ronaldo ashtuke kama kulikuwa kunamtu anamsemesha. Muda wote wakati akitafuta mbinu ya kuomba jezi ya Ronaldo, nyota huyo wa Real Madrid hakushtushwa na ombi la nahodha wa Iceland. Hii ni video jinsi nahodha wa Iceland alivyoiomba jezi ya Ronaldo
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment