
Na Baraka Mbolembole
“Hii ndiyo jezi yangu mpya. Unadhani hii ni jezi ya timu gani?” ni ujumbe ambao uliambatana na jezi inayoonekana katika habari hii.
“Sifahamu kaka, ni timu gani hiyo.” nilimjibu hivyo. Si mwingine ni mshindi mara mbili wa tuzo ya golikipa bora katika ligi kuu Bara, Shaabani Kado ambaye amemaliza mkataba wake katika timu ya Mwadui FC ya Shinyanga.
“Muda ukifika mtajua ni timu gani nitakuwa msimu ujao,” anasema Kado ambaye ataacha na kikosi hicho cha kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio.’
Kipa huyo wa zamani wa Moro United, Mtibwa Sugar, Yanga SC, na Coastal Union amepata kushinda tuzo ya kipa bora wa VPL misimu ya 2008/09 na 2014/15 aliisaidia Mwadui FC kumaliza katika nafasi ya tano msimu uliopita ikicheza VPL kwa mara ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment