SERIKALI imesema ukarabati wa kivuko
cha Mv Magogoni jijini Dar es Salaam, upo katika hatua za mwisho na
ifikapo katikati ya mwezi huu kitaanza tena kutoa huduma.
Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 2000 na magari 60 na kinatoa huduma eneo la Feri na Kigamboni.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayesimamia ujenzi),
Joseph Nyamhanga, aliyasema hayo jana alipotembelea eneo la Mamlaka ya
Bandari (TPA) linalojulikana kama ‘Dock Yard’ kuangalia maendeleo ya
uundwaji na ukarabati wa vivuko vitatu vya Mv Magogoni (cha zamani) na
vivuko vipya vya Mv Magogoni na Mv Tanga.
Nyamhanga alisema ukarabati wa kivuko
cha Mv Magogoni (cha zamani), unaendelea vizuri na upo katika hatua za
kukamilika hivyo wananchi wataondokana na usumbufu wa usafiri katikati
ya mwezi huu.
Aidha, alisema uundwaji wa kivuko kipya
cha Mv Magogoni chenye uwezo wa kubeba tani 150, abiria 800 na magari
22, unaendelea vizuri na mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 50 hivyo
Oktoba mwaka huu kitakuwa kimekamilika na kuanza kutoa huduma.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MV Magogoni kuanza kazi rasmi mwezi huu
Reviewed by Newspointtz
on
08:20:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment