Ninaweza kuachia ngoma mbili kwa mpigo August 13 – Fid Q
August 13 ni siku special kwa mashabiki wa Fareed Kubanda aka Fid Q.
Ni siku aliyozaliwa na mwaka huu ana zawadi nzuri zaidi kwao.
“Tutarajie kitu kikubwa na tofauti, watu walishajua tarehe August 13 tunaachia vitu,” ameiambia Bongo5.
“Tena stock inavyoonesha huenda tukafanya double release lakini tutatoa tu kwasababu stock ni nyingi sio labda ya pressure ya soko au nini,” ameongeza.
0 comments:
Post a Comment