Ukijaaliwa kipaji, kinachofuata ni
juhudi zako binafsi kuhakikisha unafikia malengo pia ukifikia malengo ya
awali lazima ujiwekee malengo mapya. Kama ilivyokuwa kwa Cristiano
Ronaldo, baada ya kutimiza malengo ndani ya Manchester United akaamua
kutimkia Real Madrid ambako ametimiza malengo hadi yale ambayo hakuwa
amejipangia.
AMEFANYA NINI TENA CR7?
Mfungaji bora wa muda wote Real Madrid
Cristiano Ronaldo amevunja rekodi nyingine akiwa santiago Bernabeu.
Magoli aliyofunga jana dhidi ya Valencia yamefikia 200 akicheza katika
dimba la SANTIAGO BERNABEU baada ya kucheza michezo 171 kwa misimu saba
akiwa Hispania, Magoli 149 ameyafunga akiwa katika michuano ya ligi kuu
Hispania wakati 40 akiyapata michuanao ya UEFA, mengine 10 yakipatikana
kwenye kombe la mfalme yaani Copa de rey huku goli 1 likiwa Super cup.
Ronaldo ameanza safari yake ya kufunga
katika uwanja huo akiifunga Deportivo. Lakini pia amefunga mabao mengi
kwenye mchezo dhidi ya Granada alipopiga goli 5 peke yake msimu
wa 2014/15. Mahesabu yanaonesha kasi ya Ronaldo ya kufunga ni goli 1.6
kwa kila mchezo.
Hapa Tanzania rekodi ya Mohamedi Hussein
“Mmachinga” ya magoli 26 kwa msimu mmoja inabaki kuwa ngumu kuivunja
wakati Ulaya kila mechi watu wanategemea kuvunja rekodi .
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
RONALDO ANAVUNJA REKODI ALIZOWEKA MWENYEWE
Reviewed by Newspointtz
on
07:31:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment