Tanzania,
Zambia pamoja na Jamhuri ya watu wa China zimeanza mazungumzo ya pamoja
kwa lengo la kushirikiana kuimarisha sekta ya miundombinu hususan
kufufua Reli inayounganisha Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kukuza
biashara na uwekezaji.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, amesema lengo ni kuangalia changamoto
zilizopo, ikiwemo za kisheria na kiutawala katika shirika hilo ili
hatimaye liweze kufanya kazi kwa namna iliyokusudiwa.
Awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani
zaidi ya milioni 2 za bidhaa kwa mwaka, wakati sasa inasafirisha tani
laki 2 kwa safari inayotumia hadi siku kumi na mbili kutoka Dar es
Saalam hadi New Kapiri Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.
Balozi Kijazi amesema lengo ni kuifufua
Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano
kati ya Tanzania na Zambia, kwa kuangalia umuhimu wa reli hiyo ni wa
kihistoria ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya
Watu wa China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.
Awali Tanzania na Zambia zilikubaliana
kuwekeza zaidi katika reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na
ukarabati ili kuirejesha katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza
biashara na uwekezaji.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Tanzania,Zambia kuimarisha undugu na China
Reviewed by Newspointtz
on
07:37:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment