Mchezaji nyota wa Real Madrid Gareth
Bale amekuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki sita kutokana na kusumbuliwa
na majeraha na baada ya kurejea siku ya jumamosi amekuja na njia mbadala
ya kuepuka tatizo la misuli ambalo ndio lilimweka nje kwa muda wote
lakini pengine hii njia inaweza kuwa ni ya kipekee.
Kwenye mchezo wake wa kwanza toka
amerejea siku ya jumamosi dhidi ya Celta Vigo alipachika bao lakini hiyo
haikuwa stori, utata ulikuja baada ya kugundulika kuwa anatumia soksi
iliyotoboka kwenye mguu wake wa kushoto kitu kilichofanya waandishi
wamtafute kwaajili ya kujua nini sababu ya yeye kutumia soksi yenye
tobo.
Ingekuwa hapa Bongo tayari tungekuwa na
majibu yetu kutokana na utamaduni uliopo ambao unamfanya mtu awe na
sehemu moja tu ya kuiamini kama kitu kikiwa tofauti na alivyozoea na
mara nyingi tunaamini Imani za kishirikina lakini kwa Bale mambo yako
tofauti.
Baada ya kuhojiwa Bale alisema kuwa
kutokana na tatizo la misuli kumsumbua mara kwa mara alishauriana na
daktari wake ndipo ikabainika kuwa hali ya mguu kubanwa na soksi
inasababisha misuli kukosa hewa vizuri awapo dimbani na inakuwa inavimba
taratibu ndo maana akiguswa tu ana mchezaje mwenzake misuli inavimba na
kusababisha kumweka nje ya mchezo ndo walipoamua kuja na njia hiyo ya
kuitoboa soksi ili aweze kucheza kwa uhuru zaidi huku mguu ukipata hewa
ya kutosha.
Baada ya Bale kuanza zoezi hilo siku ya
jumamosi leo pia tunatarajia kumuona na soksi yake yenye tobo mguu wa
kushoto wakati Madrid wakiwakaribisha As Roma kwenye dimba lao la
Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa marudio Uefa Champions League hatua
ya 16 bora.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
BALE ATINGA DIMBANI NA SOKSI YENYE TOBO
Reviewed by Newspointtz
on
07:08:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment