newspointtz blog
TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa
na taarifa za upotoshaji zinasombazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya
kutolewa kwa ajira mpya ya walimu kwa shule za sekondari na msingi kwa
mwaka 2015/2016.
Taarifa
hizo zinazosambazwa zinaeleza kwamba walimu wapatao 17,928 wa cheti
(Daraja IIIA) , 5,416 wa Stashahada kwa sekondari na 12,677 kwa shule
za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara wamepangwa kwa ajili ya
kuanza kazi.
Katika
taarifa hiyo inawataka walimu hao waliopangwa kuripoti kwa Wakurugenzi
wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi
tarehe 01/04/2016.
Taarifa
hizo pia zinaeleza kuwa walimu ambao hawataripoti ifikapo tarehe
10/04/2016 hawatapokelewa tena na watakuwa wamepoteza ajira zao.
Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda
kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa hizo kuwa ni za upotoshaji.
Wananchi wanapaswa kuzipuuzia kwani mpaka sasa bado Serikali haijatoa
ajira za walimu kwa mwaka 2015/2016.
Ajira
mpya za ualimu zitakapokuwa tayari zitatangazwa moja kwa moja kwenye
vyombo vya habari na katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo ni
www.tamisemi.go.tz.
Imetolewa na :
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
11/03/2016
0 comments:
Post a Comment