YANGA
SC imeendelea kukamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
baada ya sare ya 2-2 na Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Timu zote zinafikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 20, lakini Yanga inabaki kileleni mwa wastani wake mzuri wa mabao.
Timu zote zinafikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 20, lakini Yanga inabaki kileleni mwa wastani wake mzuri wa mabao.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Kennedy Mapunda, aliyesaidiwa na Frank
Komba na Soud Lilla, wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko, Yanga
walikuwa mbele kwa mabao 2-1
Azam
FC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, baada ya beki wa
Yanga, Juma Abdul Jaffar kujifunga katika jitihada za kuokoaa shuti la
mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
Hata hivyo, beki wa kulia, Juma Abdul akasawazisha makosa yake dakika ya 28 baada ya kufunga kwa shuti la umbali wa mita 20 bada ya kukutana na mpira ulioridishwa na beki wa Axam FC, Serge Wawa kufuatia shuti la Amissi Tambwe.
Mshambuliaji wa Burundi, Tambwe alipokea pasi ya Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye alianzishwia mpira wa kurusha na Mwinyi Hajji Mgwali.

Zikiwa
zimesalia dakika tatu mchezo kuwa mapumziko, mshambuliaji wa Zimbabwe,
Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili kwa kichwa akimalizia pasi ya
juu ya Tambwe.
Kabla
ya kumpasia Ngoma, Tambwe alijaribu kufunga mwenyewe baada ya kupokea
pasi ya Deus Kaseke, lakini shuti lake liliokolewa na kipa Aishi Manula
na kumrudia tena Mrundi huyo, ambaye alimuinulia Donald aliyewainua
vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 42.
Kipa
Aishi Manula a,ijitahidi kwenda kuokoa mpira huo ukiwa umekwishangia
nyavuni, lakiji haujagusa chini – hata hivyo refa Mapunda akawapa Yanga
haki yao.
Kipindi cha pili, Azam FC walirudi kwa bidii kutaka kusawazisha bao, lakini mchezo ukawa wa mashambulizi ya pande zote mbili.
Hata
hivyo, mabadiliko ya kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart John Hall
kuwaingiza wachezaji wa zamani wa Yanga kiungo Frank Domayo na
mshambuliaji Didier Kavumbangu yaliisaidia timu yake kuongeza kasi ya
mchezo.
Na
hatimaye Nahodha John Rapahael Bocco akaisawazishia timu yake dakika ya
70 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi, baada ya kupokea pasi ya Kipre
Tchetche.
Kidogo Yanga wakaonekana ‘kupooza’ baada ya bao hilo huku Azam FC wakiendelea kusaka bao la ushindi.
Kidogo Yanga wakaonekana ‘kupooza’ baada ya bao hilo huku Azam FC wakiendelea kusaka bao la ushindi.
Kuona
hivyom kocha Mholanzi akaamua kuiwekea udhibiti pointi moja, baada ya
kumuingiza beki Pato Ngonyani kwenda kuchukua nafasi ya Tambwe dakika ya
82.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva/Godfrey Mwashiuya dk68, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Pato Ngonyani dk82, Donald Ngoma na Deus Kaseke.

FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, David Mwantika, Said Mourad, Serge
Wawa, Farid Mussa/Didier Kavumbangu dk59, Jean Baptiste Mugiraneza,
Himid Mao/Frank Domayo dk68, Ramadhani Singano ‘Messi’/Mudathir Yahya
dk85, John Bocco na Kipre Tchetche.
chanzo>binzuberry
chanzo>binzuberry
0 comments:
Post a Comment