Msanii wa muziki wa bongo fleva Bob
Junior amekamatwa na jeshi la Polisi nyumbani kwao magomeni mapipa Jijni
Dar es salaam majira ya saa sita mchana wa leo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari ambaye ni rafiki wa karibu wa Bob
Junior ameiambia Mtembezi.com kuwa Polisi wamemkamata Msanii huyo kwa
kile walichodai kuwa wamepata taarifa kuwa Bob Junior anashirikiana na
kikundi cha majambazi.
Rafiki huyo wa karibu na Bob Junior,
ameiujuza mtembezi.com kuwa Msanii huyo amekuwa akipigiwa simu tangu
juzi kutoka kituo cha polisi cha magomeni usalama kwamba kuna lalamiko
la mtu anaye dai kutekwa na kikundi cha majambazi ambacho msanii huyo
anashirikiana nacho.
Unaweza kumsikiliza shuhuda wa tukio hilo na ambaye ndiye rafiki wa karibu wa Bob Junior.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
BREAKING NEWS: BOB JUNIOR ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI DAR
Reviewed by Newspointtz
on
20:36:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment