newspointtz blog
Muungano
wa Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi (Cemot) umesema hautashiriki katika
uangalizi wa uchaguzi wa marudio Zanzibar utakaofanyika Machi 20 mwaka
huu kutokana na kukabiliwa na ukata.
Cemot
ni umoja wa taasisi za waangalizi wa ndani wa uchaguzi inayohusisha
Kamati ya Uangalizi wa Uchaguzi (Temco) na Muungano wa taasisi zisizo za
kiraia za kusimamia uchaguzi (Tacceo) ambazo zilitumia waangalizi
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari Arusha katika warsha ya mrejesho wa taarifa ya
waangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu, Mwenyekiti mwenza wa Cemot,
Martina Kabisama alisema fedha zote zilitumika katika uchaguzi uliopita.
“Kwenda
kuangalia uchaguzi ni jambo linalohitaji rasilimali, hivyo hatutakwenda
Zanzibar katika uchaguzi wa marejeo kwa kuwa tulikuwa hatujaandaa
andiko la kupata fedha za uchaguzi huo,” alisema.
Kabisama alisema Cemot ilikuwa na waangalizi wa muda mfupi 9,400 na wengine 350 waliotoka Tacceo na Temco.
Mwangalizi
wa ndani wa Uchaguzi Mkuu kwa Tanzania Bara na Visiwani, Dk Alexander
Makulilo alisema Cemot ilifanya kazi kubwa katika uangalizi na
imeandaliwa taarifa inayoonyesha mahitaji ya maboresho katika chaguzi
zijazo.
Dk
Makulilo ambaye anaongoza timu ya uandishi wa taarifa ya Cemot, alisema
uchaguzi wa Zanzibar uliopita ulikwenda vizuri licha ya kuwapo dosari
kidogo sawa na Tanzania Bara.
Alisema
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na mashirika yasiyo ya kiserikali,
walifanya kazi ya kutoa elimu ya wapigakura, tofauti na Tanzania Bara.
Pia alisema visiwani humo polisi walitekeleza vizuri wajibu wao tofauti na Tanzania Bara.
Dk
Makulilo alisema asilimia 87 ya waangalizi wa Zanzibar walieleza polisi
walifanya kazi nzuri kwa asilimia 65 kutokana na kusimamia vema
uchaguzi.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment