NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Daraja la Kigamboni kufunguliwa rasmi April 2016












Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ,Profesa Makame Mbalawa amesema Daraja la kigamboni litafunguliwa rasmi April 16 mwak a huu .

Amesema kazi inayoendelea sasa ni kupitisha magari maalumu kwa ajili ya kupima ubora wa Daraja hilo ili kuridhishwa kabla ya kakabidhiwa rasmi kwa Serikali.

Hata hivyo Profesa Mbalawa amewataka watumiaji wa Daraja hilo kuwa waangalifu na kulinda miundombinu ya kuepuka vitendo vya hujuma ili lidumu kwa muda mrefuu.

“Daraja hili lina urefu wa mita 640,Barabara sita,tatu zinapanda na tatu zinashuka,hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustarabu”alisema Profesa Mbalawa

 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment