KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) aliyemaliza muda wake, Dk Richard Sezibera amewataka
wananchi kuunga mkono jitihada za kupambana na rushwa zinazofanywa na
viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake wa sasa, Rais
John Magufuli.
Sezibera aliyemaliza muda wake hivi
karibuni na nafasi yake kuchukuliwa na Liberat Mfumukeko wa Burundi,
aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa nne wa Mwaka wa jumuiya hiyo
unaofanyika Hoteli ya Hyatt, Dar es Salaam.
Alisema ili tatizo la rushwa
limalizike, hatua za dhati za kuwaunga mkono na kufichua wala rushwa
zinazofanywa na viongozi wakiongozwa na Rais Magufuli anayepambana bila
woga kukabili watendaji wanaotumia vibaya madaraka na fedha za umma.
Aliongeza kuwa, kuna umuhimu wa kila
mwananchi wa jumuiya kukataa tabia ya rushwa na ufisadi ili kuwaunga
mkono viongozi walioonesha uthubutu kukataa vitendo vya rushwa.
Katikati ya wiki hii, akiwa mjini
Arusha kuongoza kikao cha wakuu wa umoja huo, Rais Magufuli alieleza
jinsi rushwa inavyorudisha nyuma maendeleo na kuwataka viongozi wengine
wa jumuiya hiyo kuungana `kutumbua majipu’ ya watendaji wanaojinufaisha
kutokana na rasilimali za umma, badala ya kuwatumikia wananchi ambao
wengi wao ni masikini.
Mkutano huo umejumuisha makundi tofauti yakiwemo ya sekta binafsi, lengo likiwa kuzungumzia mbalimbali yanayoihusu jumuiya.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
EAC WATAKIWA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI
Reviewed by Newspointtz
on
07:24:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment