NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

EU wafikia makubalino dhidi ya wahamaiji



Viongozi wa Umoja wa ulaya walioko kwenye mkutano nchini Brussels wameamua kwa pamoja kuwasilisha pendekezo moja kuhusu Uturuki, katika kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi.

Katika mapendekezo ya mpango uliowekwa, wahamiaji wanaoingia Ugiriki kutoka Uturuki watarudishwa huku Uturuki ikipewa msaada wa kifedha na wakati huo huo raia wake kuweza kuingia barani ulaya bila visa.

Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel alilizungumzia baada ya mkutano huo wa umoja wa ulaya na Uturuki uliofanyika nchini Brussells.

Amesema Uturuki imekubali kukabiliana na umiminikaji wa wahamiaji kwa kupokea wakimbizi ambao wanarudishwa kutoka fukwe za Ugirikri ,fursa ambayo ni nzuri ili kwa kuwa inawaweka pembeni wafanya biashara haramu wa binadamu.

Hata hivyo suala hili linapaswa kuwa wazi kisheria,suala ambalo lilipewa mkazo zaidi katika mkutano huo.Tumekubaliana kuwa kila muhamiaji anayetoka katika fukwe ataweza kusikizwa yeye binafsi.

Ingawa chancellor wa Ujerumani ,Angela Merkel alisisitiza kuwa Ugiriki inahitaji msaada wakati ambao maelfu ya wakimbizi wamekwama nchini mwake.Raisi wa Ufaransa ,Francois Hollande, unahitaji makubaliano ambayo yataisaidia Ugiriki pamoja na Uturuki.


chanzo>bbc
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment