NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Jeshi la Polisi Mtwara kuimarisha ulinzi kumbi za starehe, fukwe za bahari

 
Jeshi la polisi mkoani Mtwara limewataka wananchi mkoani humo kusheherekea sikuu ya Pasaka kwa amani na utulivu na kusisitiza kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi unahimarika katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na kumbi za starehe na fukwe za bahari.
 
Akizungumza kamanda wa polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, alisema wazazi na walezi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao hawaendi kuogelea baharini kwani kwa kufanya hivyo inaweza kuwasababishia kuzama kwenye majini na kupoteza maisha.

 Aidha, amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wakuendesha vyombo vyao na kuhepuka kuendesha wakiwa wamelewa jambo ambalo linaweza kumfanya akose umakini na kusababisha ajali.

KUTOKANA baadhi ya maeneo hapa nchini kukumbwa na matukio ya ujambazi, jeshi la polisi mkoani hapa limewataka wananchi kutoa taarifa haraka iwapo watabaini kuwapo kwa watu wakigeni wanaowatilia mashaka ili waweze kuchunguzwa na vyombo vya usalama.
 
Akizungumza ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Henry Mwaibambe, alisema vilevile wananchi wanapaswa kuchunguzana wenyewe kwanza kwasababu hata wahalifu wa kigeni hawawezi kutekeleza uhalifu bila kushirikiana na wenyeji.
 
“Na vilevile ni ngumu sana mtu kutoka mbali huko na eneo lako kufanya uhalifu bila kushirikiana na mwenyeji wake, kwahiyo naomba sana tuchunguzane mienendo yetu..wiki iliyopita nilikaa na watu wa bodaboda na niliongea nao kwa kirefu sana juu ya namna gani tunaweza kushirikiana juu ya kukomesha makosa ya wizi wa pikipiki na makosa mengine..” alisema.
 
Alisema aliwaeleza mambo mengi yanayowahusu na kusema kuwa matukio mawili kati ya matatu yaliyoripotiwa polisi siku za nyuma yamewahusisha wanawake wanaokodi pikipiki kwa ajili ya kupelekwa sehemu fulani alafu baadae anaomba akajisaidie haja ndogo ndipo wanatokea vijana na kupora pikipiki.
 
“Ni mtu tu anakodi pikipiki nipeleke Naliendele njiani anasimamisha ili akajisaidie kidogo haja ndogo, wanajitokeza vijana wanapora pikipiki..sasa ni vyema unapochukua hiyo pikipiki kwenye kundi la watu mufahamiane vizuri, sio rahisi mtu akapora pikipiki yako bila kujua mwenendo wako, sasa hata mienendo yetu inabidi tuiangalie vizuri nawaombeni sana..” aliongeza Mwaibambe.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment