Tangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli
alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje,
Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais
aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.
Rais Magufuli alizuia safari za nje siku
chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa
wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni
mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.
Tangu wakati huo, safari za nje kwa
watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara
za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Jana, Rais Magufuli aliwaruhusu mawaziri
wawili kwenda Vietnam kujifunza mbinu za kuinua kilimo na kujenga
viwanda ili kuwaondoa Watanzania kwenye lindi la umaskini.
Mawaziri wawili waliopata kibali hicho
ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba.
Rais Magufuli alitoa uamuzi huo jana
baada ya kufanya mazungumzo na Rais Truong Tang Sang wa Vietnam juzi na
kukubaliana kuweka sawa mazingira ya biashara na uwekezaji baina ya nchi
zao.
Akizungumza jana baada ya kumtembeza
Rais huyo kwenye Eneo Maalumu la Uwekezaji la Benjamini Mkapa (EPZ)
lililopo Ubungo jijini hapa, Waziri Mwijage alisema Dk Magufuli ametoa
kibali hicho baada ya kuridhishwa na mabadiliko ya muda mfupi ya
Vietnam.
“Kutokana
na hatua waliyopiga, Rais ameniruhusu mimi na Waziri wa Kilimo, Mwigulu
Nchemba kwenda nchini humo muda mfupi baada ya Rais Truong kuondoka. Alisema Mwijage.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
JMP ARUHUSU MAWAZIRI WAWILI SAFARI YA NJE
Reviewed by Newspointtz
on
11:18:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment