Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (MB) amekifungia kiwanda cha kuzalisha cement na chokaa kilichopo jijini Tanga cha Rhino Cement, jana jioni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni uharibifu na uchafuzi wa mazingira na kuvunja sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Mh.
Mpina amechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
wananchi wa kata ya maweni kupitia diwani wa kata hiyo Bw. Joseph Colvas
na kujionea mwenyewe namna ambavyo kiwanda hicho kinavyo achilia moshi
mzito kwenda angani, pamoja na vumbi lisilovumilika kusambaa katika
maeneo ya makazi ya wanachi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaa
katika maeneo ya shule ya sekondari ya Don Bosco ambapo, Mh. Mpina
ameelezwa kuwa athari zitokanazo na uachiachi wa hewa hiyo chafu angani
si tu kwa watoto wa shule zinazozunguka kata hiyo bali pia ni kwa viumbe
hai na mazingira.
Kwa
upande wake Afisa Afya wa jiji la tanga aliyejulikana kwa jina moja la
bwana Kizito alimuelezea Naibu Waziri Mpina kuwa ni kweli kiwanda hicho
kimekuwa kikifanya uchafuzi huo wa mazingira, na Afisa uendeshaji kutoka
Baraza la Taifa na HIfadhi ya Mazingira NEMC Bw. Novatus Mushi ameeleza
kuwa kiwanda hicho kimeshawahi kutozwa faini ya shilingi milioni kumi
na saba (17) kwa kosa la kuchelewa kulipa ada ya mwaka ya mazingira
pamoja na uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa na kiwanda hicho kwa
upande wa kuzalisha chokaa.
Mh.
Mpina ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (
NEMC) kukifunga kiwanda hicho kisiendelee na uzalishaji kwa muda
usiopungua miezi mitatu, na kulitaka baraza hilo lijiridhishe na
kufuatilia namna kiwanda hicho kinavyotakiwa kutekeleza sheria ya
mazingira kwa kujenga mfumo wa kisasa wa kutoa taka zitokanazo na
uzalishaji kiwandani hapo pamoja, na kupima vumbi na moshi utokao
kiwandani hapo kama hautakuwa na madhara na athari kwa mazingira na
viumbe hai. Kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa moja kwa moja.
Aidha,
akitolea mfano wa kiwanda cha bonite bottles cha mjini moshi kwa kuwa
kinara katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira, mh Mpina alivitaka
viwanda vingine viige mfano wa kiwanda hicho cha coke cola.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment