Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi
wake ''Kuchati'' katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda
wa saa za kazi.
Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.
Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.
Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.
chanzo>BBC
0 comments:
Post a Comment