NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

LIVE KUTOKA TAIFA: SIMBA 1 VS NDANDA FC 0



Dk 40 Ntebe anafanya kazi ya ziada, anaokoa mpra mbele ya miguu ya Kiiza inakuwa kona. Simba wanapiga lakini haina manufaaa
Dk 39, Mponda anapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya kupiga kichwa butu akiwa karibu kabisa ya lango la Yanga
GOOOOOOOO Dk 36, krosi safi ya Kessy, Kazimoro anaunganisha vizuri na kuifungia Simba bao la kwanza

Dk 33, Green anapiga kichwa, kinampita kipa wa Simba, wakati mpira unakwenda kujaa wavuni. Majabvi anaokoa
KADI Dk 31 Ntebe analambwa kadi ya njano kwa kuutupa mpira kwa makusudi
Dk 30, Ntebe anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira na kuwa kona kwenda Ndanda.  Lufunga anapiga kichwa safi lakini mpira unapita juu
Dk 27 krosi safi ya Kazimoto kabla haijamfikia Ndemla, Majabvi anaugusa mpira na kumpoteza maboya mwenzake. Wanapoteza nafasi tena

Dk 26, Kazimoto anajaribu kupiga shuti. Analenga lango lakini ni shuti dhaifu
DK 21 hadi 25, Simba wanaonekana kushambulia zaidi lakini bado inaonekana Ndanda wako makini zaidi katika ulinzi na hakuana hofu hata kidogo.

Dk 19, Kiiza anajaribu kupiga shuti lakini ni dhaifu
DK 17, Ndemla kwa mara nyingine anapiga shuti lakini anashindwa kulenga
Dk 15, Simba wanafanya shambulizi tena, krosi safi ya Ajib, Kiiza naye anampasia Kessy, anapiga krosi safi hata hivyo Ndanda wanaokaoa
Dk 12, Ndemla anaingia vizuri na kupiga shuti kali lakini linapita juu kidogo ya lango
 
Dk 9, Majabvi anapiga shuti lakini linakuwa dhaifu na halilengi lango
Dk 7, Tshabalala anapiga krosi lakini inaonekana kuwa dhaifu, kipa anadaka kwa ulaini. Mechi inaonekana kuchezwa zaidi katikati ya uwanja
Dk 4, Atupele Green anajaribu kupiga shuti, lakini anabutua kabisa
Dk 1, mechi inaanza taratibu kila upande ukionekana kuusoma mwingine kwa umakini
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment