WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi ameagiza watumishi watatu wa Idara ya Ardhi
katika Halmashauri ya wilaya ya Monduli, kupandishwa kizimbani kutokana
na tuhuma za wizi wa fedha za halmashauri hiyo.Wanadaiwa
kuuza viwanja zaidi ya 200 kati ya Sh milioni mbili hadi nne bila
kuingiza fedha hizo katika akaunti ya halmashauri hiyo.
Lukuvi alitoa
agizo hilo juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Francis Miti kwenye
mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake wilayani humo, baada wananchi
kutoa malalamiko yao ya kuuziwa viwanja hewa na watumishi wa
halmashauri.
Watumishi wanaotuhumiwa ni Ofisa Ardhi
Mteule wa wilaya hiyo, Kitundu Mkumbo ambaye ni Mpimaji wa ardhi ,
Leonard Haule pamoja na Mchora Ramani, Leonard Mkwavi. Lukuvi alisema
kuwasimamisha kazi watumishi hao haitoshi hivyo ni vyema wakafikishwa
mahakamani kwa kukiuka maadili ya watumishi wa umma pamoja na kurudisha
fedha zote za wananchi hao waliowatapeli kwani wanalipa stakabadhi za
halmashauri.
Aidha aliagiza ofisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na polisi katika wilaya
hiyo, kufanya uchunguzi wa haraka na wa kina kisha kuwafikisha
mahakamani watumishi hao.
Akipokea maagizo hayo, Mkuu huyo wa
wilaya alisema baada ya kutambua ubadhirifu huo aliagiza watumishi hao
kuwekwa ndani kwa saa 24 pamoja na kuwasimamisha kazi. Alisema uchunguzi
huo umeshaanza na kwamba uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani
mara moja.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM ) wilaya ya Monduli, Loota Sanare alimuomba waziri
kufikisha ombi lao kwa Rais Dk John Magufuli kufuta hati za mashamba 39
ambayo yapo katika wilaya hiyo lakini wawekezaji wanayoyamiliki
hawayaendelezi.
Akiwa wilayani humo, Lukuvi alikabidhi
mashamba makubwa 13 kwa wananchi wa wilaya hiyo ambayo Rais Magufuli
aliyafutia hati kutokana na wamiliki kutoyaendeleza kwa muda mrefu.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
LUKUVI ‘AWATUMBUA JIPU’ MAAFISA ARDHI WA MONDULI
Reviewed by Newspointtz
on
06:47:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment