NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Makonda Awapa Wiki Mbili Watendaji wa Kinondoni Kuhakikisha Mashimo Yote Yaliyopo Barabarani Yanazibwa


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alifanya ziara ya kukagua barabara ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza baada ya kukagua barabara hizo alisema amewapa watendaji wa manispaa ya Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya magari yanayotumia barabara hiyo.
"Sasa nimeiagiza Manispaa, nimewapa wiki mbili kuhakikisha mashimo yote yawe yamezibwa, na wakishindwa nitawasaidia kuwawajibisha na kuchukua hatua stahiki." Alisema Paul Makonda

Alisema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Makonda alisema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanaotumia barabara hiyo.


chanzo>mpekuzi
 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment