TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza, imemfikisha mahakamani aliyekuwa Meya
wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata (63) na wenzake wawili wakikabiliwa
na mashitaka ya kutumia vibaya madaraka.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo
waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya
Nyamagana ni aliyekuwa Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Justine Lukaza
(42) na mfanyabiashara Hemedi Hamad (54).
Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Mwema
Mella, alidai mbele ya hakimu Greyson Sumaye kwamba kati ya Juni mosi na
Julai 31, mwaka 2014, washitakiwa hao walitumia vibaya madaraka kwa
kutoa zabuni ya kutoza ushuru katika Kituo cha Mabasi cha Buzuruga
kinyume cha utaratibu.
Alifafanua kuwa makosa waliofanya ni
kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
mamba 11/2007 na pia walikiuka sheria ya manunuzi ya umma namba 7/2011
Wakati kesi hiyo inafikishwa mahakamani jana, mshitakiwa Lukaza
hakuwepo, hatua iliyomfanya Mwendesha Mashitaka kuomba mahakama hati ya
kumkamata.
Hakimu aliridhia ombi hilo na kesi hiyo
ilioahirishwa hadi Machi 29 mwaka huu. Washitakiwa wawili waliokuwepo
mahakamani walikana mashitaka hayo na wako nje baada ya kutimiza
masharti ya dhamana
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MEYA WA ZAMANI ILEMELA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Reviewed by Newspointtz
on
09:23:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment