MGANGA wa tiba za asili, Juma Ramadhani
pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha Utalii Masai, Saumu Mohamed (19)
wanashikiliwa na Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma za kuharibu mimba ya
miezi saba.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Mihayo
Msikhela aliwaambia waandishi wa habari jana, watuhumiwa hao ambao ni
wakazi wa mtaa wa Sahare, walikamatwa Februari 29 mwaka huu saa 2:00
usiku katika mtaa huo ulio kata ya Mzingani.
Alisema kukamatwa kwao kumekuja baada
ya wananchi kuokota maiti ya mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike ambaye
inadaiwa alikuwa ni mimba ya miezi saba.
“Siku hiyo ya tukio katika maeneo ya
Sahare jijini Tanga aliokotwa mtoto wa kike ambaye ni mimba ya miezi
saba. Inadaiwa mimba hiyo iliharibiwa na Saumu ambaye in mwanafunzi wa
Chuo cha Utalii Masai cha mkoani hapa”.
Alisema na kuongeza: “Binti huyo
kulingana na uchunguzi wetu wa awali anadaiwa kunywa dawa ya kutoa mimba
kwa kutumia dawa maalumu ambayo alipewa na mganga wa kienyeji aitwaye
Juma Ramadhani na ndipo ikaharibu ujauzito huo na kisha Saumu
alipofanikiwa kujifungua, akaamua kutupa maiti ya mtoto huyo ambayo
baadaye iliokotwa na wananchi.”
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa na Polisi na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MGANGA WA JADI AKAMATWA AKIMTOA ‘DENT’ MIMBA YA MIEZI SABA
Reviewed by Newspointtz
on
09:24:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment